Thursday, April 28, 2011

Mdau Anauliza; " Hivi, Gamba Ni Nini?"


Salaam,
Nimekuwa nikifatilia mijadala vijiweni,magazetini,TV shows kama Je tutafika,chanel10 on monday,Kasongo n.k.

Kama sijakosea bado sijasikia watu waki-define neno gamba au kwanini ccm wanasema wamejivua gamba kwani gamba linatatizo gani?,na ni nini haswa..?kama gamba ni umri tuambiwe,kama gamba ni ufisadi tuambiwe ni wa kiasi gani cha fedha kinachohusishwa na madhara yake ni yapi kiuchumi,kijamii n.k mfano ufisadi huu unahusishwaje na vifo vya kina mama kwa kukosa huduma za uzazi na Je kuna taratibu zozote za kisheria juu ya ufisadi huo? ili pasiweze jirudia tena. Je ndg Nape kisha eleza kifasaha juu ya ufisadi huo?

Ukisema unawafukuza katika nyadhifa ndani ya ccm hao mafisadi pasipo kuhusisha taratibu za kisheria/mahakamani unakuwa umetimiza maana kamili? Je ni busara kumfukuza/kumuondoa mtaani kwenu jirani yenu mwizi/muuaji pasipo kumfikisha mahakamani? huoni kuwa uatakuwa ni mshirika wake yaani unaona ilimradi atakuwa hatoki au si jirani yako tena basi hata kama ataendelea na wizi/uwaji wake kwako hakuna tatizo.

Ni vema kina Nape/ccm/sie tujadili madhara ya ufisadi huo katika jamii yetu yaani tuelimishwe kina dowans n.k wameiathili kwa kiasi gani jamii yetu.
Mdau.

No comments:

Post a Comment