MIAKA 47 YA MUUNGANO BAK KI MOON AMTUMIA SALAMU ZA PONGEZI RAIS
JAKAYA KIKWETE NA WATANZANIA-
NA MWANDISHI MAALUM
NEW YORK
Wakati watanzania wakiadhimisha hapo kesho miaka 47 ya Muungano.Katibu Mkuu
wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki Moon amemtumia salamu za pongezi Rais wa Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania, Jakaya Mrisho Kikwete, Serikali na watanzania wote.
Katika salamu zake ambazo nakala yake ilitumwa katika Ubalozi wa Tanzania Umoja
wa Mataifa, Ban Ki Moon anasema , wakati huu kuliko ilivyokuwa wakati mwingine
wowote, dunia inakabiliwa na changamoto nyingi.
Amesema changamoto hizo ambazo zimevaa sura tofauti na uzito tofauti, zinavuka
mipaka kutoka taifa moja hadi lingine. Na kwamba kuzitafutia ufumbuzi kunataka
utulivu, umakini, mshikamano na ushirikiano wa kimataifa .
Katibu Mkuu huyo wa Umoja wa Mataifa, amemwelezea Rais Jakaya Kikwete kwamba,
yeye binafsi amedhamiria katika kuhakikisha kuwa Umoja wa Mataifa, unakwenda
sambamba na kasi ya mabadiliko yanayotokea hivi sasa duniani. Na kuhakikisha
kwamba Umoja wa Mataifa unasimamia na kutoa matarajio yenye kuridhisha na halisi
katika kazi zake tatu kuu za msingi ambazo ni maendeleo, amani na usalama na haki
za binadamu.
Ameeleza kuwa anafarijika na kutiwa moyo sana na uongozi unaojituma wa
ya Muungano wa Tanzania . Na kwamba anaihesabu Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania kama mshirika mkubwa katika kuifanya dunia kuwa endelevu na salama
kwa watu wote.
|
No comments:
Post a Comment